Posts

KWANINI CHIZI HAUMWI?

 Umeshawahi kujiuliza kwanini chizi haumwi anapokula vitu vichafu lakini mwenye akili huwa anaumwa anapokula vitu vichafu? Je unadhani ni kipi kinachomfanya mgonjwa wa akili asiumwe wakati yeye ana mwili kama wako na ana tumbo kama lako? Kitaalamu mtu anapokuwa ana tatizo la akili, yaani hana akili vizuri kuna baadhi ya hofu huwa zinaondoka kwenye akili yake. Huwa hafikirii matokeo ya alichofanya, ila huwa anafanya anachoona sawa kufanya kwa wakati huo anaofanya. Chizi au mgonjwa wa akili huwa haumwi kwa sababu hana hofu ndani ya moyo wake, ndio maana hapati madhara kama anayopata mtu timamu anapofanya kitu cha madhara. Hofu ndio adui mkubwa na anaweza kukutengenezea maradhi hata sehemu ambayo haina maradhi. Licha ya kuwa dunia inapitia kwenye changamoto ya maradhi hatari ya Corona, lakini hofu pia inachangia idadi ya vifo kuongezeka. Sikwambii usichukue tahadhari hapana, chukuwa tahadhari ila ondoa hofu. Hofu ndio inayokufanya ushindwe kufanikiwa miaka yote kwa sababu unaamin...

MAISHA NA MISIMU YAKE

BWANA mmoja aliwaitisha wanawe wanne, na kuwapa somo juu ya kujifunza kutokuhukumu mambo kwa haraka. Akawataka waende, kwa awamu, nchi moja ya mbali kuuzuru mti mmoja uliopandwa miaka takribani thelathini nyuma. Walikwenda kwa awamu tofauti, na waliporejea wote, kila mmoja alitakiwa atoe ushuhuda. Mtoto wa kwanza akasema: ameuona mti, lakini ulikua hauvutii; umepinda, mbaya na matawi yake yanayumbishwa na kutupwa na upepo. Mtoto wa pili, akampinga mwenziye kwa kusema ameuona mti ni mzuri; umependeza una maua mazuri na majani ya kijani. Mtoto wa tatu naye akasimama na kusema: ameuona mti.ulikuwa mbaya na umekauka...hauna majani wala maua.haukumpendeza Mtoto wa nne aliposimama, akashangaa majibu ya wenzake.yeye akasema ameuona mti ukiwa umezaa matunda makubwa na matamu.mti ulikuwa ukinukia majani yaliyochanua. Baada ya wote kutoa ushuhuda, baba akawaambia wanawe kuwa wote walikuwa sahihi, kwa sababu kila mmoja ameuona mti,lakini walitofautiana kwakuwa waliuona kwa misimu to...