Posts

Showing posts from May, 2020

MAISHA NA MISIMU YAKE

BWANA mmoja aliwaitisha wanawe wanne, na kuwapa somo juu ya kujifunza kutokuhukumu mambo kwa haraka. Akawataka waende, kwa awamu, nchi moja ya mbali kuuzuru mti mmoja uliopandwa miaka takribani thelathini nyuma. Walikwenda kwa awamu tofauti, na waliporejea wote, kila mmoja alitakiwa atoe ushuhuda. Mtoto wa kwanza akasema: ameuona mti, lakini ulikua hauvutii; umepinda, mbaya na matawi yake yanayumbishwa na kutupwa na upepo. Mtoto wa pili, akampinga mwenziye kwa kusema ameuona mti ni mzuri; umependeza una maua mazuri na majani ya kijani. Mtoto wa tatu naye akasimama na kusema: ameuona mti.ulikuwa mbaya na umekauka...hauna majani wala maua.haukumpendeza Mtoto wa nne aliposimama, akashangaa majibu ya wenzake.yeye akasema ameuona mti ukiwa umezaa matunda makubwa na matamu.mti ulikuwa ukinukia majani yaliyochanua. Baada ya wote kutoa ushuhuda, baba akawaambia wanawe kuwa wote walikuwa sahihi, kwa sababu kila mmoja ameuona mti,lakini walitofautiana kwakuwa waliuona kwa misimu to...